Pata Namba ya Kumbukumbu ya Malipo/Control Number (99111xxxxxxx) baada ya kujisajili ambayo utaitumia kulipa TZS 30,000.00 kwa mkupuo mmoja kwa njia zifuatazo:
MPesa, AirtelMoney,Halopesa, T-pesa, Ezypesa au TigoPesa kwa kuchagua malipo ya Serikali. Baada ya kulipa, utatumiwa stakabadhi yako kwa njia ya ‘sms’; Au,
Tumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo/Control Number uliyopata kutoka katika mtandao wa OLAMS kufanya malipo katika Tawi lolote au Wakala yeyote wa Benki za TPB, CRDB na NMB. Ikiwa una swali, muulize Afisa wa Benki.